\ talktz

Mabibi na mabwana ! Video: Alikiba – Chekecha Cheketua

Zilipita pichaz na vipisi tu lakini hii ndio video kamili ya Ali Kiba ‘chekecha‘ ambayo imefanywa South Africa wiki kadhaa zilizopita… ukishaitazama uache maoni yako kwenye comment Ali Kiba na team yake watapita kuona nini mashabiki wanasema.


‘Chekecha Cheketua’ iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu. Video imeongozwa na Meji Alabi.

Majibu ya Zari kwa wanaomshutumu kutoheshimu Mwezi wa Ramadhan yanashtua

Zari the Bosslady amejikuta kwenye kitimoto kutokana na mashabiki kumshambulia mtandaoni kwa mavazi yake katika mwezi mtukufu wa Ramadhan.Mama huyo mtarajiwa wa mtoto wa Diamond amelazimika kutumia Kiswahili kuwajibu wale wanaomshambulia kwa mavazi yake katika kipindi hiki ambacho waislamu duniani kote wapo kwenye mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.
“Mnikome, maisha yangu yanakuhusu nini wewe, na yako hayanihusu mimi kabisa ata kidogo,” ameandika Zari kwenye Instagram.
“Oh sijui high heels, mara nguo imembana, sijui anapikia heels,pili pili hujakula wewe inaakuwashia nini? Mvae madera zenu mfunge mkanda mpite kimya kimya. Kwanini unastress???? HAYA NI MAISHA YANGU,”ameongeza.

“Na sasa your all Gods’ judges now…. how many people do we know that wear hijab but have very dirty ugly hearts? Huh? How many of you act so straight for these 30 days but the last 11 months you’re the worst monsters this world has ever seen. Now u wana come here and judge my faith by the dress?”

“Allah bless all of you….atleast I ain’t acting snitchy, am being ME. And oh, if you happen not to like what you see in ur news feed (my page) U always have 3 options, Block yourself, unfollow ama fast forward coz if your still following na you exercise your fingers kuwakya matusi page yangu, babe your just an obsessed fan if not a confused admirer dah majirani. Habari nakazi mnayo……like I always say, no bad vibes from me. So stay blessed.”

VIDEO- Kwataharifa yenu hainiumi ”NG ‘O”- Ommy Dimpoz

Baada ya msanii Ommy Dimpoz kupost Instgram Atwek ya AliKba  ailiyo zungumiza siku itakayo tambulisjhwa kichupa hicho ,mashabiki walinza kumporomoshea matusi ya nguoni .Ommy Dimpoz amewajibu kwa kupitia video hii .


”sasa ndugu zangu tuki post wasanii wenzetu mnatukana,tukikaa kimya tuna roho mbaya tufanyeje ???Matusi tu hamjali kama watu wana wazazi wengine wamekufa rakini kwa taharifa yenu hainiumi ”Ngo”. Ommy Simpoz

”Cheketua ” kuzinduliwa Trace Tv 29 june

alikiba1Mkali wa Bongo fleva AliKiba aka King Kiba ,kichupa chake cha ”Chekecha Cheketua ” kuzinduliwa  jumatuu hii katika kituao kibubwa duniani cha Tv ”Trace Tv” mashabiki wa AliKiba kaeni mkao wa   kupata kukiona kichupa hicho


WEMA SEPETU: Siwezi Kumsapoti Diamond Platnumz Kwenye Mtv Awards Kwasababu Nitaonekana Ninajipendekeza,,,

Katika Kipindi cha TV cha Wema Sepetu Kiitwacho In My Shoes Wema  Amedai kuwa hawezi Kumsapoti Mwanamuziki Diamond kwenye Tuzo za Mtv Awards kwa vile Kufanya Hivyo ataonekana anajipendekeza kwa vile Diamond hajawahi kumuomba kufanya hivyo…
Pia amedai kuwa yeye na Diamond walishayamaliza hivyo hataki kujihusisha na Diamond kwa njia yoyote ile kama ni kosa alishalifanya kipindi cha nyuma na hawezi rudia kosa..

Katika hatua nyingine Wema Sepetu amedai kuwa Kitendo cha yeye kumsapoti Ali Kiba katika tuzo za Kill Music kilikuja baada ya Ali Kiba yeye Mwenyewe Kumuomba Wema Kufanya Hivyo na kumtumia picha ambazo alizipost kwenye Account yake ya Instagram….

source Darcitycenter.com

Christian Bella adai amembadilisha Alikiba kwenye collabo yao

Christian Bella aka King of the best melodies amedai kuwa kazi yake mpya na Alikiba itakuwa na utofauti mkubwa kwakuwa Kiba amebadilisha kwenye wimbo huo.


Akizungumza na  Bongo5  leo, Bella amesema Kiba ni msanii aliyeweza kwenda naye sambamba kwenye kupanda na kushuka kwa sauti.

“Nimefurahi jinsi tulivyoelewana masauti humu ndani,” amesema Bella.

“Nimemfanya sasa Alikiba kuimba na mimi akaonyesha kiwango kingine baada ya kukaa na king of the best melodies. Nilinyoosha melody na yeye ikabidi atembee vile vile, njia niliyopita mimi pick za juu sana na yeye akapita humo humo pia. Yaani imekuwa nzuri sana yaani kinoma. Kwahiyo ngoma ipo tayari,” ameongeza.

Hata hivyo muimbaji huyo amesema bado wimbo huo haujapewa jina.

“Jina na wimbo bado halijakamilika lakini baada ya leo ndo tutajua unaitwaje,” amesisitiza Bella.

“Sasa hivi tunajipanga kuhusu video na video ikikamilika baada ya mwezi wa ramadhani ngoma itatoka. Sitapenda ichelewe kwa sababu mashabiki walikuwa wanasumbua tufanye kolabo na Alikiba na ndo umefika muda wao kupata kile walichohitaji. Ingawa imechukua muda kutokana na sisi sote kuwa busy, kwahiyo mipango iliyobaki ni video ili tutoe video pamoja na audio na video tutafanya video kubwa kwa ufupi tu na sidhani kama tutashoot hapa nchini.”
alimalizia Bella.

Jinsi Wema Sepetu na Jokate Mwegelo walivyozungumzia ushindi wa Alikiba!

Ushindi wa Alikiba kwenye tuzo za KTMA 2015 haujatokana na nguvu ya Team Kiba tu bali pia nguvu ya Wema Sepetu na Jokate Mwegelo na majeshi yao.


Alikiba na Jokate wanadaiwa kuwa na uhusiano. Wema amekuwa upande wa Kiba tangu kuachana na Diamond na wengi wamekuwa wakikichukulia kama ni kisasi.

Baada ya ushindi huo warembo hao walitumia Instagram kutoa pongezi zao.

“Hongera sana cherie @officialalikiba kwa kujishindia tuzo sita jana usiku kwenye kiba Tanzania music awards (KTMA) sorry Kilimanjaro Tanzania music awards 2015. Teh teh the,” aliandika Jokate.

“Ni kitu cha kumshukuru Mungu ulikaa kimya miaka 3 ila ukarudi na wimbo mmoja ukatuteka tena. Kusema ukweli tukiachilia mbali ushabiki ‘mwana’ ulituliza akili na ukafanya vizuri sana nchini. Mashabiki wanakupenda. Sana. Mpole hivi, mcheshi, mstaarabu. Na unajua mziki. Tunakuombea sasa hii iwe motisha ya wewe kufika mbali zaidi. Ndio kwanza safari imeanza. Uzuri unaomba mungu so najua hata kutupa. Ila kaza mwana we kazaaa!!! We are behind you,” aliongeza.

Naye Wema aliandika: Nilitaka zote saba ila hata 6 pia sio mbaya…. #KingKiba…. Umetisha.”

Jokate pia amepost picha akiwa na Wema na kuandika: It’s a beautiful and powerful thing when strong girls come together. emojiemojiemoji️. With The Sweetheart @wemasepetu.”

Mr Blue amshukuru mke wake kwa kumsaidia kuacha kutumia bangi,sigara,mirungi na pombe.

Kupitia kurasa ya instagram ya Mr Blue, msanii huyu ameweka shukurani zake kwa mke wake Wahyda kwa kumsaidia kuacha kuvuta bangi, sigara, kula mirungi na kunywa pombe. Blue aliandika hivi.


Video ya Yemi Alade “Pose” yuko na Mugeez wa kundi la (R2Bees).

Hii video mpya ya Yemi Alade “Pose” aliofanya na msanii kutoka Ghana Mugeez wa kundi la (R2Bees). Video imetayarishwa na muongozaji kutoka Ghana Paul Gambit na kufanyika Nigeria na Ghana.

 
Support : talktz | Shau Template | Mas
Copyright © 2011. talktz - All Rights Reserved
Template Modify by Shau
Proudly powered by Blogger